Monday, 4 November 2013

MABADILIKO MAKUBWA MITIHANI YA SEKONDARI

-DIVISHENI ZIRO YAFUTWA
-  VIWANGO VYA UFAULU VYASHUSHWA
Wanafunzi wa Kidato cha nne wakiwa wameanza mtihani siku ya leo ya tarehe 4 Novemba, 2013, Serikali imepunguza alama za ufaulu kwa mtihani huo pamoja na ule wa Kidato cha Sita.

Pia imetangaza kuwa, mitihani ya taifa wa vidato hivi tajwa hapo juu utakuwa na alama 60 za ufaulu, huku alama 40 zilizobaki zitatokana na zile za maendeleo ya mwanafunzi shuleni zinazojulikana kama CA.

Katika mfumo huo mpya, wizara hiyo pia imefuta daraja la sifuri na badala yake kutakuwa na daraja la tano
.  Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome alitangaza uamuzi huo wa Serikali siku ya Alhamisi kwa kueleza utekelezaji wa utaratibu huo utakaoanza kwenye mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne mwaka huu.

Profesa Mchome alisema kuwa "Hatua hii imechukuliwa kutokana na changamoto zilizojitokeza kuanzia mwaka 2011 kwa hiyo tangu wakati huo kumekuwa na mabadiliko mbalimbali ambayo yamekuwa yakifanyika".

Alisema kuwa, alama zilizokuwa zikutumiwa awali na Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) katika kupanga matokeo hayo kwa kidato cha nee na 
A=80-100, B=65-79, C=50-64, D=35-49, F=  0-34

"Alisema mfumo mpya, umeshusha alama za kidato cha nne na cha sita na kuanzia sasa A=75-100, B+=60-74, B=50-59, C=40-49, D=30-39, E=20-29 na F=0-19, akieleza kuwa Alama A itakuwa ni ufaulu ulijipambanua, B+ utakuwa ni ufaulu bora sana, B ufaulu mzuri sana, C ufaulu mzuri, D ufaulu hafifu, E ufaulu hafifu sana na F ufaulu usioridhisha kabisa,"alisema Profesa Mchome.

Alisema pia kuwa, "wamebadilisha mfumo wa madaraja ambao awali kulikuwa na daraja la kwanza, la pili, la tatu, la nne na sifuri, lile la sifuri tumeliondoa, badala yake kutakuwa na daraja la tano, lengo ni kuweka mlolongo mzuri zaidi" alisema.

MAONI YA WADAU
katika mchakato huu wadau wa secta ya elimu wameipongeza Wizara kwa kuamua kutumia CA lakini wasiwasi mkubwa ni kwamba jambo ambalo linatakiwa kufuatiliwa kwa umakini mkubwa ni uhakikishaji wa wa alama hizo zinazoonyesha uwezo halisi wa mwanafunzi, kwa sababu mwaka 2011 wale wanafunzi walioandika vitu visivyoeleweka kwenye mitihani yao ya mwisho kwenye CA walikuwa wana mpaka alama 75, kwa hiyo hapa tunaona kutakuwa na ugumu gani katika nyanja hii.

Na kuhusu kushusha kiwango cha ufaulu ni kwamba, tusishushe viwango vya ufaulu kwa wanafunzi ili waweze kufaulu kwa wingi ila Wizara ipaswa kuhakikisha ya kwamba wanafunzi wanapata elimu bora mashuleni.

0 comments:

Post a Comment