Ads 468x60px


Featured Posts

Monday, 4 November 2013

MABADILIKO MAKUBWA MITIHANI YA SEKONDARI

-DIVISHENI ZIRO YAFUTWA
-  VIWANGO VYA UFAULU VYASHUSHWA
Wanafunzi wa Kidato cha nne wakiwa wameanza mtihani siku ya leo ya tarehe 4 Novemba, 2013, Serikali imepunguza alama za ufaulu kwa mtihani huo pamoja na ule wa Kidato cha Sita.

Pia imetangaza kuwa, mitihani ya taifa wa vidato hivi tajwa hapo juu utakuwa na alama 60 za ufaulu, huku alama 40 zilizobaki zitatokana na zile za maendeleo ya mwanafunzi shuleni zinazojulikana kama CA.

Thursday, 26 September 2013

TUKIO LA UGAIDI KENYA

Mwandishi wa habari wa Gazeti la New York Times la Marekani, Tyler Hicks, aliyeshuhudia tukio la kigaidi lililofanywa na Kundi la Kigaidi la Al Shabaab katika jengo la Westgate, jijini Nairobi, Kenya amesema hali ya mambo ilivyokuwa ni ya hatari kuliko hata kuandika habari za vita vya Syria, Afghanistan, Iraq au eneo lingine lolote la vita duniani.
http://api.ning.com/files/x19830JkrtNNbAxxKot2X2h0QDFMmsl2n6cZxl*GiJDiKdYa1fPum0gvp9LhwNSlOPCyW2mseDoO6DnIGRPWFT1lHpaziZuQ/MAUAJIKENYA18.jpg
Wananchi waliokuwa ndani ya jengo la Westgate wakiokolewa.

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara akutana na wadau wa muziki na sanaa za maonesho